04 Jul 2022
Kuhusu Rijk Zwaan
Uzalishaji wa mboga
Rijk Zwaan ni kampuni ya kimataifa ya uzalishaji wa mbegu za mboga yenye makao yake makuu nchini Uholanzi. Wafanyakazi wetu ni takribani 3,800 kwenye nchi 30 tofauti wanaona kazi ya kuongeza thamani kwenye bidhaa na kutoa huduma kwa washirika wetu ni ya kufurahisha na kuridhisha sana.
Mpangilio wa Kampuni
Familia tatu zinamiliki takribani asilimia 90% ya hisa zote za Rijk Zwaan. Asilimia 10% ilinayobakia humilikiwa na kundi kubwa la wafanyakazi kupitia ununuaji wa hisa kwa wafanyakazi. Kila mwaka, kila mfanyakazi ana nafasi ya kununua hisa na kushiriki kifedha katika Rijk Zwaan.
Maono ya Muda Mrefu
Rijk Zwaan ilikua na itaendelea kua Kampuni inayojitegemea. Tumejiridhisha kua Mashirika ya aina hii yanatoa fursa nzuri za kuanzia kwa kipindi cha muda mfupi na mrefu. Hali ya washikadau kuendelea kama kampuni inayojitegemea, pamoja na utamaduni wa kampuni, unawapa wafanyazi wa Rijk Zwaan ulimwenguni kote motisha ya kufanya kazi.
Nafasi za masoko
Rijik Zwaan ni moja ya makampuni 4 bora katika soko la mboga na humiliki asilimia 9. Tumechagua kuangalia zaidi kwenye mbegu za mboga na utoa wigo mkubwa ndani ya sekta hii.
Mpangilio wa mauzo
Kwa kuuza mbegu zetu, tumechagua mfumo wa asili. Mbegu zetu huuzwa zaidi ya nchi 100 na kupitia matawi ya ndani yapatayo 30. Kwenye nchi mabazo hatuna matawi yetu wenyewe, tunafanya kazi na wasambazaji. Makampuni yote haya hufanya kazi katika soko maalumu yakizingatia hali ya hewa na hali ya soko katika eneo husika.
Uvumbuzi
Ili kuendeleza aina mpya ya mbegu na usambazaji wa mbegu zenye ubora wa hali ya juu, uvumbuzi endelevu ni muhimu. asilimia 40 ya wafanyakazi wenzetu wanajihusisha na utafiti na kila mwaka tunawekeza asilimia 30 ya mapato yetu kwenye tutafiti huu.
Sinema ya Kampuni
Kuangalia filamu fupi nenda www.rijkzwaan.com kwa maelezo zaidi