Mbinu za mawasiliano
Ushauri wa muda halisi
Orodha yetu ya mazao pamoja na hali ya kilimo huwa vinabadilika-badilika. Hali hii inalazimu ushauri uende na wakati, mara nyingi ukihusisha watu walio mbali. Ndiyo maana tunatumia mbinu za mawasiliano za masafa marefu. Pamoja na ushauri mahsusi na binafsi, mbinu hizi zinakusaidia kupata taarifa endelevu kuhusu bidhaa mpya zinazoingizwa sokoni pamoja na vidokezo vya kilimo.
Tunazichukulia simu mahiri (smartphones) kama chombo muhimu cha kuwafikia na kuwasaidia wakulima barani Afrika, na kwa sababu hii tunaendelea kubuni mbinu mpya zinazoingiliana za simu za mkononi. Kwa mfano, tunatumia MFarming kutangaza mbegu zetu na kutoa vidokezo vya kilimo, na kwa kupitia mitandao ya kijamii ya maeneo husika tunatoa vidokezo vya mapishi ya vyakula na taarifa kuhusu siku za maonyesho . Wateja wetu wanapata huduma zetu kupitia programu yetu ya "Rijk Zwaan apps".
Unaweza kutarajia nini kutoka kwetu?
- Orodha ya bidhaa zetu kwenye tovuti yetu
- Katalogi ya Rijk Zwaan Afrika
- Vipeperushi na magazeti maalum
- Ushauri mahsusi kwa wateja kupitia njia (portal) ya wateja wetu ya Partner RZ
- Ujumbe wa Facebook + WhatsApp na huduma za SMS (kwa Tanzania tu)