Kiswahili Kenya

19 Nov 2021

Chapisho la Blogu

Labda unajua kwamba Rijk Zwaan ni kampuni ya kuzalisha mbegu za mboga mboga yenye makao yake Uholanzi, na kwamba Rijk Zwaan imeorodheshwa kama nambari 4 duniani kwa mbegu za mboga mboga, lakini unajua kwamba Rijk Zwaan pia ni kampuni inayomilikiwa na familia?

Watu wenye motisha kubwa

Rijk Zwaan ni mojawapo ya makampuni makubwa yaliyosalia yanayomilikiwa na familia katika sekta ya Mbegu. Asilimia tisini ya hisa zinamilikiwa na familia tatu ambazo zote bado zinafanya kazi katika kampuni, , na hisa zilizobaki zinashikiliwa na kundi kubwa la wafanyakazi. Rijk Zwaan alikuwa, yupo na daima atakuwa biashara inayojitegemea. Tunauhakika kuwa aina hii ya biashara inatoa mahali pazuri pa kuanzia kwa mafanikio katika muda mfupi na mrefu. Uamuzi wa wanahisa kuendelea kama kampuni inayojitegemea, , pamoja na utamaduni wetu maalum wa kampuni, inaunda motisha kubwa kwa zaidi ya wafanyikazi 3600 wa Rijk Zwaan kote ulimwenguni.

Karibu na soko

Rijk Zwaan huwekeza karibu 30% ya mauzo yetu katika Utafiti na Maendeleo kila mwaka, na tunauza mbegu zetu za mboga mboga katika nchi zaidi ya 100. Tunaamini katika mbinu za ndani, na katika kila hali kampuni zetu tanzu na wasambazaji hufanya kazi katika soko mahususi na kuzingatia hali na mahitaji ya ndani.

Historia

Je! ungependa kujua jinsi Rijk Zwaan ilifikaje hapa ilipo, tangu Bw Rijk Zwaan alipoanzisha kampuni hii karibu miaka 100 iliyopita mnamo 1924? Tafadhali tazama video hii fupi ili kujifunza kuhusu safari yetu.