Kiswahili Kenya

02 Jan 2022

Mafanikio na Loleza RZ F1

Rijk Zwaan Afrisem inafanaya tafiti nakuzalisha Pilipili Mbuzi. Lengo ni kutengeneza aina za Pilipili Mbuzi zenye mavuno mengi na ukinzani kwa usalama bora wa mazao. Kuna mkazo mkubwa kwenye ukali lakini pia juu ya harufu, kukomaa haraka na maisha bora ya baada ya kuvunwa.

Kutembelea shamba la Farm Land

Tulitembelea Farm Lands, kampuni iliyoko Arusha, Tanzania ili kusikia kuhusu uzoefu wao na Loleza RZ F1. Qambarali Ladha mwanzilishi alituambia: “pilipili hii ya Kiafrika inashangaza kwa jinsi inavozaliana, ubora na mavuno mengi. Hakika ndiyo pilipili kali zaidi!”

Kutoka kilimo cha hobi hadi kibiashara

Qambarali : “Shamba letu lilianza kama shamba la hobi ambalo sasa limegeuka kuwa la biashara inayokua kwa lengo la kuzalisha mazao bora katika shamba la ekari 8 (hekta 3,2) ambapo ekari 1.5 zinatumika kwa pili pili mbuzi ya Loleza RZ F1”.

Safari kutoka kuota hadi kuvuna

“Mbegu zetu chotara kutoka kwa Rijk Zwaan kila mara hupandwa kwenye kitalu kwa lengo la ubora na ufanisi, na huota kwa angalau asilimia 95 ya Mbegu zote. Mchakato huu wa Loleza ulichukua siku 21 - 25, upandikizaji ulifanyika tarehe 29 mwezi wa Tisa 2021 wakati safari hii ilianzia kwenye uwanja wazi. Licha ya msimu wa kiangazi kutoka mwezi wa Tisa hadi mvua za Mwezi wa kumi na mbili, mimea hii iliendelea kuwa na afya bila kujali hali mbaya ya hewa. Wafanyakazi wa Rijk Zwaan walitembelea mara kwa mara na waliweza kushuhudia ukuaji wa miche na kiwango cha uzalishaji,” anasema Qambarali.

Kutoka shambani hadi kwa wateja

Qambarali anasisitiza kuwa katika shamba la Farm Lands uzalishaji ni muhimu lakini ubora ndio muhimu zaidi! Tunajitahidi sana kuongeza mavuno kwa kila mmea kwa kuzingatia njia sahihi za utunzaji wa mmea, kwa kutumia umwagiliaji kwa njia ya matone na kulisha mmea kwa mbolea za maji. Hivi ndivyo Farm Lands inavyopata matokeo mazuri kwa wastani wa gramu 8.5 kwa kila tunda, umbo zuri la kufanana lakini lenye mwonekano wa kuvutia na ladha nzuri ya pili pili inayothaminiwa na wateja wao wanaopatikana katika masoko ya ndani ya Tanzania, Kenya na Ulaya.

Sikia kutoka kwa Qambarali mwenyewe

Unataka kujifunza zaidi katika maneno ya Qambarali mwenyewe? Kisha tafadhali tazama video hii