Kiswahili Kenya

11 May 2022

Ngogwe/ Nyanya Chungu

Holland Greentech, ni wasambazaji rasmi wa mbegu za Rijk Zwaan nchini Rwanda. Hivi majuzi waliandaa hafla ya kutambulisha Kazinga RZ F1, aina ya Ngogwe au Nyanya chungu.

Mbegu za Ngogwe au Nyanya Chungu.

Ngogwe ni zao maarufu nchini Rwanda, ikiwa ni mboga ya nne kwa mauzo ya mazao baada ya nyanya, vitunguu na kabichi. Hata hivyo, wakulima wengi, karibu na Rwanda, wanapanda Ngogwe kwa kutumia mbegu zilizozalishwa kutoka kwa mazao ya awali, zenye uwezo mdogo wa uzalishaji. Holland Green Tech na Rijk Zwaan walitambua hitaji la kuanzisha aina ya mbegu chotara iliyoboreshwa. Kazinga RZ F1, ina mmea wenye nguvu na mavuno mengi, matunda yana rangi nyeupe ya kuvutia na maisha marefu baada ya kuvunwa.  https://www.rijkzwaanafrica.com/sw-ke/node/26456

Siku ya Maonyesho.

Maonyesho ya Kazinga RZ F1 yalifanyika Kagitumba, Wilaya ya Nyagatare. Eneo linalojulikana sana lililoko katika jimbo la Mashariki mwa Rwanda, eneo hili linajulikana sana kwa kilimo cha mboga mboga, ambapo wakulima wengi wakiwemo wauzaji mboga mboga nje ya nchi hupanda mboga  mboga mwaka mzima. Siku ya shamba darasa  iliandaliwa kwa ajili ya wakulima, wauzaji bidhaa za mboga mboga nje ya Nchi, mawakala wa ugani na watendaji wengine wanaojihusisha na kilimo cha bustani kuona utendaji wa zao hilo na kupata ujuzi wa usimamizi wa Kazinga RZ F1.

Kazinga RZ F1: Mshangao...!

"Martha" ambaye ni mmoja wa wakulima waliohudhuria siku ya shamba darasa, na ambaye ana kiwanja, karibu na shamba darasa alielezea kushangazwa kwake na Kazinga RZ F1, na kusema kuwa, "ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona aina ya Ngogwe kama hii. Watu wazima na watoto waliifurahia kwa sababu haina uchungu, ina matunda mengi, na inastahimili magonjwa ukilinganisha na mbegu za bilinganya za Kiafrika tulizokuwa tukizikuza. Ni aina nzuri sana na itakuwa chaguo langu kwa msimu ujao."

Kuona ni kuamini.

"Daniel" mkulima aliyesimamia shamba la maonyesho, alikuwa na haya ya kusema, "Nina furaha sana kutokana na faida niliopata kutoka kwenye kiwanja cha majaribo cha 0.5 hekta. Alisema “Nilikuwa nalima mboga nyingine ambapo mbali na umwagiliaji na kurutubisha, bado nilitakiwa kuwekeza sana kwenye ulinzi wa mimea, lakini kwa aina hii sikuwekeza sana na sasa nipo mwishoni mwa mwezi wa tatu. navuna na kama unavyoona bado navuna”

Je, una unashauku ya kuajribu kilimo hichi katika nchi yako? Tafadhali tafuta mwakilishi wa eneo lako hapa https://www.rijkzwaanafrica.com/sw-ke/mawasiliano