Kiswahili Kenya

Msaada kwa mkulima

Rijk Zwaan inaendeleza mboga chotara tu. Mbegu hizo zina faida nyingi kubwa:
• Mavuno mengi zaidi
• Mavuno ya mapema zaidi
• Ustahamilivu dhidi ya magonjwa na wadudu waharibifu
• Siha nzuri ya mimea
• Maisha marefu ghalani
• Ukuaji wa haraka
• Ubora wa hali ya juu na ulingano wa zao

Ukulima wa mboga unahitaji ushauri mahsusi. Ndio maana uhusiano wetu na wakulima ni zaidi ya kuuziana mbegu tu. Ni muhimu kwetu kuhakikisha kwamba mbegu zetu chotara zitatoa matokeo bora, na ndiyo maana tunatumia muda mwingi na jitihada katika kutoa ushauri wa kilimo na mauzo.

Je, unatafuta aina tofauti ya mbegu?

Angalia aina mbalimbali zinazopatikana kwenye ukanda wako
Kwenda kitabu cha bidhaa