Ushuhuda wa Bertha

‘Kutoa mbegu mpya chotara ni jambo la kuridhisha sana’

Bertha Beganyi ameifanyia kazi Rijk Zwaan tangu 2014. Jukumu lake ni kuchagua pilipili kali. Anaweza kutumia jukumu hili kuendelea kutoa mbegu mpya, hivyo kulisisimua soko – na wakati mwingine hata kujisisimua mwenyewe.

Rangi na maumbo

"Nilisomea mikrobayolojia na botania, ambayo ilinipa msingi kamili wa kazi ninayofanya sasa. Kuna aina nyingi sana za pilipili! Wakati wa kutengeneza mbegu mpya chotara, wakati mwingine matokeo huwa ya kushangaza sana kwa msingi wa rangi na maumbo. Lakini lazima tuzingatie zaidi ya haya. Kwa mfano, wadudu wa aina ya thiripi ni tatizo kubwa sana kwa wakulima, sawa na virusi kama vile CMV na PVY. Kwa kukuza uwezo asili wa kustahimili, tunaweza kupunguza matumizi ya kemikali kulinda mazao na kufanya kilimo cha mboga cha Afrika kuwa endelevu zaidi."

Upendeleo wa Breeder

"Ili kufanya chaguo sahihi za uzalishaji, ni muhimu sana kushirikiana. Kuna maelezo mengi sana ambayo tunahitaji kushughulikia, na ili kufanikiwa, tunahitaji usaidizi wa kila mtu! Wakati huo huo, kuna kile ninachokiita 'upendeleo wa mhamili (breeder)'. Wakati mwingine unahitaji kutii silka yako na kujaribu jambo jipya. Hakika, huu ni mwanzo wa mpango huu wa uzalishaji. Bado kuna mengi ya kuchunguza..." 

 

Changamoto

"Mwisho wa yote, jambo linaloridhisha zaidi ni kutoa aina mpya ya mbegu sokoni, ambapo inaweza kuwasaidia wakulima kuwa na mafanikio zaidi. Mimi pia huwatembelea wakulima mwenyewe ili kutumia mawazo yao kufanya maboresho zaidi. Lakini wakati mwingine ni vigumu kupata wakati wa kutosha. Hakika, huenda mimea mpya iko tayari kwa kufanyiwa utathmini na haitakusubiri!"

 

Pata aina inayokufaa