Ushuhuda wa Marco (World Vegetable Center)
'Benki ya vinasaba isiwe makumbusho'

Marco Wepereis (katikati kwenye picha) ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Mboga (World Vegetable Centre – WorldVeg), taasisi isiyo ya kifaida ya kimataifa ya tafiti na maboresho mahsusi kwa ajili ya mboga. Anakubaliana na mtazamo wa Rijk Zwaan kwamba mboga zina nafasi muhimu katika maendeleo ya Afrika.
Utaalam
“Hapa World Vegetable Center tunakabiliana na umasikini na utapiamlo kwa kuchochea uzalishaji na ulaji wa mboga zenye lishe. Bado kuna mengi ya kuendeleza, hususan barani Afrika – si kwa kusaidia idadi kubwa ya wakulima wadogo kwa kuwapatia vianzilishi na utaalamu tu, bali pia kwa kuanzisha mifano ya ushirika na kuimarisha mifumo ya thamani. Hii inaweza kukuza soko la ajira kwa kiwango kikubwa, hususan kwenye maeneo ya kando ya miji. Shughuli za kibiashara hunufaisha wadau wote!”

Uwekezaji wa muda mrefu
“Bila shaka, mbegu bora ni moja ya mahitaji muhimu. Ndiyo maana tunafurahi tunapoona kampuni ya uhamili kama Rijk Zwaan ikiwekeza kwa mtazamo wa muda mrefu. WorldVeg ina benki kubwa ya vinasaba kuliko zote duniani, ambayo ni wazi kwa kila mtu, yenye kabila zaidi ya 60,000 kutoka takriban nchi 145. Hata hivyo, benki yetu ya vinasaba haipaswi kuwa makumbusho, na ndiyo maana tunajitahidi kujenga mahusiano na sekta ya uhamili. Tuna shauku ya kuona kampuni hizo zikitumia malighafi yetu kuboresha aina za mboga – kama vile kuboresha uwezo wa kustahimili magojwa au halijoto zaidi.
“Wakati huo huo, Rijk Zwaan inaweza kutupatia taarifa muhimu kuhusu hali yalisi ya mahitaji. Unaweza kugundua ukweli wa kile kinachohitajika pale unapofanya kazi kwa ukaribu zaidi na wakulima – kama vile jinsi ustahimilivu dhidi ya magonjwa mapya ulivyo muhimu, kwa mfano. Lakini, kampuni za uhamili pia hukabiliwa na changamoto za usambazaji katika kuhakikisha kwamba walaji wana chanzo cha kuaminika cha mboga za ubora wa juu.”
Kufikia kikomo cha uwezo
“Tuna mipango kabambe, hasa kule kusini mwa Asia na Afrika ambako ulaji mdogo wa mboga unadumaza maendeleo wa mamilioni ya watoto. Unawazuia wasifikie kikomo cha uwezo wao, kitu ambacho hakiwezi kurekebishwa baadae na hakisameheki. Tunataraji kuona ongezeko kubwa la mahitaji ya mboga jinsi miji inavyokuwa haraka. Hatupaswi – na hatuwezi – kutegemea kukidhi mahitaji hayo kwa kuagiza (mboga) kutoka nchi nyingine, kwa hiyo iko haja ya kujenga taaluma hiyo katika maeneo hayo. Ndiyo maana miradi ya ushirikiano baina ya sekta binafsi na mashirika kama WorldVeg ni ya muhimu sana.”
Soma zaidi kuhusu Ushirikiano na miradi