Ushuhuda wa Alioune

'Fursa za mauzo kwa wakulima ndani ya nchini'

Alioune Ndiaye anafanya kazi katika kampuni ya Agroseed, wasambazaji wa mbegu za Rijk Zwaan nchini Senegal. Ubora wa mboga zinazopatikana nchini humo tayari unaridhisha, lakini bado kuna fursa nyingi zaidi. Viwango vipya vya ubora na aina mpya za mboga zinaweza kuwainua wakulima kwa kiasi kikubwa.

Hamasa

 “Hapa Senegal tunakula sana mboga, mchana na jioni. Hali yetu ya hewa ni nzuri kwa uzalishaji wa mboga za ubora wa hali ya juu; nyingi zikiuzwa Ulaya na wawekezaji wakubwa wa kigeni. Kwa muda mrefu utaalamu wa kilimo cha bustani ulihodhiwa na wataalamu wachache walioajiriwa na makampuni hayo makubwa na haukuwanufaisha wakulima wadogo.Lakini hali inabadilika sasa; wasenegali wengi zaidi wanagundua fursa zilizopo kwenye kilimo hich na wanaanza kuhamasika.”

 “Chukuwa tikitimaji, kwa mfano. Hali yetu ya hewa inaruhusu kuyalima kutoka Oktoba mpaka wakati wa pasaka. Viwango vya jua na joto huwa muafaka kwa kilimo cha matunda ya ubora wa hali ya juu na yenye sukari nyingi. Ni majuzi tu ndiyo tumeanza kuuza mbegu zake kwa wakulima.”

Soko la ndani

“Ili kuwasaidia tumefungua shamba la maonyesho huko Soleil Vert Gorome 1, ambako tunaonyesha mboga za aina mbalimbali za Rijk Zwaan. Inawaonyesha wakulima wigo mpana wa mboga na faida za ustahimilivu dhidi ya maradhi na uhifadhi mrefu. Wakiimarisha ubora wanaweza kuuza zaidi kwenye soko la ndani linalokuwa na kusafirisha nchi za jirani kama vile Mauritania na Guinea.”

“Kazi yangu inaridhisha sana. Nafurahia sana kuhudumia mimea nikishirikiana kwa ukaribu na wakulima.  Hivi karibuni tulianza kutumia utaratibu wa karatasi za tathmini ambao umetuwezesha kudhihirisha mafanikio. Hii ni muhimu kwa sababu napenda kuuza kule tu ambacho najua ni kizuri.”

Pata aina inayokufaa