Ushuhuda wa Ben, Kees na Marco

'Kujituma'

Tanzania ina nafasi maalum mioyoni mwetu. Hii ilianza mwaka 2002 tulipoanza kuzalisha mbegu pale Arusha. Tulichagua eneo hilo kwa sababu ya hali yake nzuri ya hewa kwa uzalishaji wa mbegu za ubora wa juu. Tulipotembelea Afrika Mashariki tulishuhudia kwa macho yetu ubaya wa mbegu zinazotumiwa na wakulima na utaalam mdogo wa wakulima wengi wadogo. Tukataka kuona kama tunaweza kutumia utaalam wetu kuboresha hali hiyo.

Hatua za kwanza za utafiti

Pamoja na East West Seeds, kampuni yenye uzoefu mkubwa wa kuhamili mboga katika nchi za joto za barani Asia, tilichukuwa hatua za kwanza za majaribio kwa kushirikiana na Mpango wa Mbegu za Mboga Tanzania (Tanzania vegetable Seed Program – TVSP) kati ya 2005 na 2007. Nia ilikuwa kupata picha ya vikwazo vilivyopo kwenye mnyoyoro wa ugavi wa mbegu na kupima aina zilizopo kwa matumizi katika Afrika Mashariki. Vile vile, wakulima walipata mafunzo ya awali kwa kiwango kidogo. Tulijifunza jinsi uzalishaji wa mboga unavyoweza kuwapatia wakulima wadogo kipato kizuri na kukuza uchumi wa eneo hili.

Muda mrefu

Mwaka 2008 mradi huo ukabadilika na na kusababisha kuzaliwa kwa Rijk Zwaan Afrisem, ambayo lengo lake kuu ni kuipatia sekta ya kilimo cha bustani barani Afrika mbegu za ubora wa juu za aina chotara. Soko la mbegu zinazozalishwa na mkulima (Farmer Saved Seeds – FSS) na aina zinazochavushwa wazi (Open Pollinated Varieties – OPV) bado ni kubwa sana lakini, kama ilivyoainishwa kwenye utamaduni wa kampuni yetu, tumechagua kuwa na malengo ya muda mrefu.

Mbegu na huduma

Tunajivunia kwa kuanzisha mpango (programu) wa kwanza ya kuhamili mboga chotara za mboga mahsusi kwa soko la Afrika Mashariki. Lakini tunaelewa pia kwamba aina bora pekee hazitoshi. Uzoefu wetu huko ulaya na Asia umetuonyesha kwamba elimu na mafunzo kwa wakulima ni muhimu ili kuendeleza sekta ya mboga. Sisi tunauita mtazamo huo ‘mtazamo wa mbegu na huduma’. Tumejikita kuleta mtazamo huo barani Afrika pia

Soma zaidi kuhusu Uhamili kwa ajili ya Africa