Ushuhuda wa Robert

'Kuona ni kuamini'

Robert Tiemtoré hufanya kazi ya ukuzaji wa bidhaa kwa niaba ya Rijk Zwaan nchini Burkina Faso. Hapa, watu wanapenda mboga sana, lakini viwango vya utaalam wa kiufundi wa wakulima viko chini sana. Mbinu ya asili inahitajika ili kuboresha hali hii. Ukiachilia mbali kuchagua aina ya asili humu nchini, changamoto kuu ni kufikia idadi kubwa ya wakulima wadogo wadogo.

Hali za kiasili

"Nilipokuwa mtoto, nilitumia muda mwingi nikifanya kazi katika shamba la wazazi wangu. Hili lilinitia motisha kujifunza zaidi kuhusu mbinu za kilimo, kwa hiyo nilienda kusoma katika Chuo cha Kilimo cha Bobo. Hapa nilijifunza umuhimu wa maji safi na uwezo wa kustahimili magonjwa, miongoni mwa mambo mengine. Ningependa kutumia maarifa yangu kuchangia katika juhudi za kukabiliana na ukosefu wa chakula na maendeleo ya sekta ya mboga nchini mwetu."

Maboresho

"Njia kuu ninayotumia kuboresha mbegu ni kupima aina mpya katika mashamba ya wakulima, ili ziweze kujaribiwa katika hali za kieneo. Mojawapo ya malengo yetu ni kuanzisha aina zinazokomaa mapema ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ndogo tu, na viwango vipya vya maji; mambo ambayo hupunguza bei zake za kukuzwa, na kwa hiyo huzalisha mapato bora kwa wakulima zinapouzwa. Kiwango kikubwa cha mavuno huuzwa na wanawake ambao huyasafirisha hadi masoko ya nchini, lakini mazao ya ubora wa juu pia yanaweza kuuzwa nje ya nchi katika mataifa kama vile Kodivaa au Ghana." 

Maendeleo taratibu

"Kwa kutembelea wakulima wengi tofauti, nimeshuhudia mambo ambayo mbegu na huduma hufanya. Ubora wa mazao umeongezeka na matatizo yanayosababishwa na magonjwa yamepungua zaidi. Hata hivyo, bado kuna changamoto kubwa ya kuwafikia wakulima wengi wadogo wadogo. Mkakati wetu ni kupata wakulima wenye motisha katika maeneo yote muhimu. Hivi majuzi tulifanya jaribio dogo la aina mpya ya mbegu. Liliwavutia wakulima wengi kutoka eneo hili ambao wote walitaka kujua jinsi ya kudhibiti ubora wa aina hii. Huu ndio utaratibu tunaotazamia kwa kwa sababu, kama wasemavyo, kuona ni kuamini."

Soma zaidi kuhusu Msaada kwa mkulima