Ushuhuda wa Dokun

'Ongezeko la kuvutiwa na ubora wa mboga'

Dokun Ogunbodede anamiliki kampuni ya biashara ya kilimo nchini Nigeria, ambapo yeye huchanganya uzalishaji mboga, ushauri na maoni ya usambazaji ya wakulima wengine. Kwa kipindi cha miaka michache iliyopita, amekuwa akifanya kazi na Rijk Zwaan. Pamoja, wanaona uwezo mkubwa wa kilimo nchini Nigeria.

Mazao freshi

"Mwaka wa 2014, nilijenga nyumba ya kwanza ya kulimia (greenhouse) nchini Nigeria. Kwa usaidizi na mbegu za Rijk Zwaan, niliweza kuzalisha mboga za ubora wa juu. Watu wameanza kupenda mboga pole pole, lakini itachukua muda kukuza soko. Hususan, kizazi kipya kinazidi kupenda masuala ya afya na bidhaa zenye ubora. Kwa sababu ya watu zaidi ya milioni 170 nchini, kuna nafasi mkubwa sana ya biashara."

 

Changamoto ya hali ya hewa

"Ili kutimiza uwezo huu, ni lazima kukabiliana na changamoto chache kubwa nchini Nigeria. Kwanza, joto na baridi ya hali ya hewa inaathiri ukuzaji mazao. Aidha, kuna ukosefu wa maarifa na upungufu wa pembejeo. Sekta yote ina maendeleo duni, na ndiyo sababu tunataka kushirikiana na makampuni mengine na kujifunza kuhusu matukio katika nchi nyingine. Pia tutapanua ushirikiano wetu na Rijk Zwaan: hivi karibuni pia tutaanza kuuza mbegu zao." 

Uvumilivu na motisha

"Nina hamu sana ya kushiriki katika kuleta mabadiliko katika sekta ya mboga nchini mwangu. Kwa sasa, Nigeria huagiza bidhaa nyingi za mboga kutoka sehemu nyingine za dunia, kama vile Asia, Ulaya na Afrika Kusini. Lakini nina imani kwamba Nigeria ina uwezo wa kuzalisha mazao yake pia. Katika miaka michache iliyopita, nimejifunza kinachohitajika haswa: vifaa, mbegu na ushauri unaolingana na hali ya nchini, na juu ya yote uvumilivu na motisha mwingi sana. "

 

Soma zaidi kuhusu Uhamili kwa ajili ya Afrika