Ushuhuda wa Dominique

'Uwekezaji mdogo, matarajio makubwa'

Dominique Emanuel ni mgeni katika kilimo cha mboga. Hivi karibuni, aliwekeza katika "greenhouse" ndogo katika kijiji chake cha Moshono na kupata ushauri wa kitaalamu kutoka Rijk Zwaan. Matokeo ya kwanza yalikuwa yanatia moyo na na sasa, akishirikiana na mwanae, ana matarajio makubwa kwa siku za usoni.

Uwekezaji

“Nilikuwa nafanya kazi ya udereva katika kampuni ya utalii hapa Arusha lakini siku zote nilikuwa na hamu ya kufanya shughuli za kilimo. Nikaamua kuanzisha kuanza na ufugaji wa kuku lakini nilihangaika kupata mafanikio. Wakati wa Nanane (sikukuu ya kitaifa ya wakulima) nikakutana na watu wa Rijk Zwaan; wakanishawishi kuingia kwenye kilimo cha mboga. Nilikuwa na akiba ndogo ya fedha benki na mshauri wao alinishauri niiwekeze kwenye kilimo cha ndani.  Nilimwamini na nikajenga greenhouse ndogo.”

Vidokezo muhimu

“Rijk Zwaan walinishauri nianze na pilipili. Greenhouse yangu ilinipa fursa ya kuwahi kuingia sokoni, kitu ambacho kilinisaidia kimauzo. Kilimo cha mboga kilikuwa jambo geni kwangu lakini nilikuwa na Rijk Zwaan nyuma yangu, hata baada ya kununua mbegu. Kwa kupitia ziara za washauri wao na  vidokezo vya whatsapp walinipa ushauri muhimu kuhusu upogoaji na uwekaji wa mbolea, na pia kuhusu umuhimu wa usafi na muda muafaka wa kunyunyizia dawa. Katika mwaka wa kwanza niliweza kuvuna kilo18 kwa kila mita ya mraba. Kwa kuuza mazao yangu sokoni niliweza kurejesha gharama zangu haraka sana.”

Biashara inayokuwa

“Kwa sasa mwanangu anasomea shahada yake ya kwanza katika masoko lakini tayari anajua kwamba itambidi arithi biashara hii. Tunaamini kwamba kilimo cha mboga kina mustakabali mzuri kwa siku zijazo hapa Tanzania. Ndiyo kwanza tumejiunga ha TAHA, chama cha wakulima wa mboga Tanzania, ambacho kinaweza kutusaidia katika mipango yetu ya kuuza mazao yetu huko Kenya. Na bado tuna ardhi tupu kubwa tu kando yetu. Tunaiona greenhouse hii kama ‘mama’ na tunataraji kwamba “atazaa” watoto wengi tu baadae...!”

Soma zaidi kuhusu Msaada kwa mkulima