Maono ya Kees, Ben na Marco

Watu ndio Kiini

Wanahisa na wakurugenzi wanaamini lengo kuu la kampuni ni kuwapa wafanyakazi wao kazi ya kufurahisha na ya kudumu kwa masharti mazuri ya ajira. Lengo hili kuu ni msingi ambao wafanyakazi wote kwa kushirikiana na washirika wengine wanachangia kwenye afya ya kizazi kijacho.

Utamaduni wa kampuni

Kazi ya kufurahisha inahitaji mazingira mazuri na yenye kutia moyo, hii ndiyo sababu tunaona tamaduni ya kampuni yetu ni muhimu sana. Vipengele muhimu vya tamaduni yetu ni kama ifuatavyo:

• Uaminifu
•Moyo wa ujasiriamali ikitoa nafasi kwa wigo wa ubunifu na uvumbuzi.
• Maadili ya Biashara ya hali ya juu.
• Mazingira mazuri yanayoletwa na uwazi na ukweli, kuheshimu wengine, moyo wa kufanya kazi na wengine na kiwango kikubwa cha maadili.

Uaminifu tulionao kwa wafanyakazi wetu unarudishwa kwa motitsha kubwa, kujitolea kwa hali ya juu na ushirikiano mkubwa ambao kwa inatuletea faida kubwa kwa wateja, wasambazaji na sekta mbalimbali za serikali pamoja na washirika wetu wengine. Wote wanaweza kumtegemea mtu mwaminifu, mwenye bidhaa zenye ubora na huduma nzuri.

Uongozi wa Rijk Zwaan: Kees Reinink, Ben Tax and Marco van Leeuwen