Uhamili kwa ajili ya Afrika
Rijk Zwaan iko Afrika kote. Ili kuendeleza uwezo halisi wa bara hili muhimu, tuna mtazamo wa muda mrefu. Tumewekeza kwenye kituo cha uhamili na kwa makusudi kabisa tumechagua kuendeleza aina chotara tu.
Lengo
Kilimo cha mazao chotara kinahitaji umakini mkubwa wa wakulima katika uwekezaji, lakini kina faida kubwa kutokana na mazao mengi na bora zaidi. Ili kuisaidia sekta ya mboga barani Afrika ikuwe kunahitajika aina bora (za mboga), utaalamu mzuri na subira nyingi. Hii itawapa wakulima wadogo nafasi muhimu katika ujenzi wa chanzo endelevu cha chakula barani Afrika. Lengo letu ni kusaidia katika ukuaji wa ongezeko la upatikanaji wa mboga zenye lishe na kuwasaidia wakulima wa Afrika kuinua kipato chao.
Rijk Zwaan Afrisem
Katika kituo chetu cha uzalishaji cha Rijk Zwaan Afrisem huko Arusha, Tanzania, tunahamili mboga chotara za kiafrika: ngogwe, sukuma wiki na pilipili mbuzi. Tunahamili pia nyanya fupi. Vile vile, aina nyingine za mboga kutoka mabara mengine zinatathminiwa ili kubaini uwezo wake wa kulimwa katika maeneo ya Afrika Mashariki na Afrika Magharibi. Tumeajiri wafanyakazi 70 na tuna hekta 20 za ardhi ya kilimo, ikijumuisha mashamba ya majaribio, mabanda ya kulimia (greenhouses) na vitalu vya kutenga (isolation blocks) vyenye viwango vya kisasa vya Rijk Zwaan. Shamba letu la maonyesho linatuwezesha kuonyesha na kutathmini wigo wetu (wa mazao) na mbinu zetu za kilimo mwaka mzima.
Mtazamo wa kibiashara
Mbegu zetu barani Afrika huuzwa kupitia kampuni zetu tanzu za mauzo (huko Afrika Kusini, Moroko, Misri na Tanzania) na mtandao mkubwa wa wasambazaji na wasimamizi wa mauzo. Katika maeneo mengi wakulima bado wako katika kujifunza mbinu bora za kulimo cha mboga. Ndiyo maana tuna timu maalum ya washauri wa kilimo wenye uzoefu inayolenga kuwajengea uwezo huo. Kwa vile wako katika kitovu cha soko husika (washauri hao) wanaweza kutoa ushauri wa kitaalamu unaoendana na hali halisi.