Ushirikiano na miradi
Kuendeleza kilimo cha bustani katika Afrika ni kazi kubwa na ngumu inayohitaji ushirikiano wa wadau kadhaa katika sekta hiyo. Kwa hiyo, tuko tayari kushirikiana na kampuni, taasisi na watu binafsi wenye lengo kama letu. Tunaona ushirikiano na wadau wa mahali husika kama sharti muhimu ili tufanikiwe.
Kusambaza maarifa ya kiufundi
Wakulima wa Afrika wana mahitaji mengi zaidi ya aina bora za mboga. Kiukweli, aina bora ni mwanzo tu kwa vile kuna vitu vingi vya kuendeleza katika kuboresha taaluma na mbinu za mauzo. Kwa vile tunahitaji wingi na uwepo wa wataalamu katika eneo husika ili kuongeza mafanikio, tunajitahidi kujenga ushirikiano na asasi za kiserikali, vyama vya wakulima na taasisi za mafunzo barani kote. Tunafurahi tunapochangia ujuzi wetu na utaalam katika miradi ya muda mrefu kama vile AIM, SEVIA, Horti-Impact na Smart.
Kuendeleza soko pamoja
Bado kuna mambo mengi ya kuendeleza katika kilimo cha bustani barani Afrika katika nyanja za mbinu za ugavi (logistics), usimamizi wa fedha, ubora, masoko na ujasiriamali. Kwa kuwa karibu na mkulima tunataka kuwapa uzoefu wetu na kubadilishana mawazo na serikali, wagavi wa mboga, taasisi za mikopo midogo na wadau wengine. Kama moja ya shughuli zetu tunajaribu kuwaunganisha wakulima na mabenki, wagavi na taasisi za masoko ili waweze kuendesha biashara zao kwa utaalam zaidi. Hatimaye jamii zao pia zitanufaika kwa kukuwa kwa uchumi.
Kuhamasisha ulaji wa mboga
Ulaji wa mboga ndiyo njia endelevu zaidi ya kupambana na ukosefu wa virutubisho. Ili kuhamasisha ulaji wa mboga barani Afrika, tunatambua kwamba ni muhimu kuwa na aina za mboga za jadi zinazohimili hali ya hewa ya pale. Kwa hiyo, tunatumia vianzilishi (vya mimea) kutoka katika taasisi kama vile Kituo cha Mboga cha Kimataifa (World Vegetable Center). Vile vile tunajiunga na miradi kama vile Amsterdam Initiative against Malnutrition (AIM) ambayo inaunganisha wadau mbalimbali ili kuimarisha usalama wa chakula na lishe kupitia wigo mpana wa miradi.