Kiswahili Kenya

19 Mar 2020

Virus vya Corona – Rijk Zwaan inachukua tahadhari madhubuti zinazotuwezesha kuendelea na uzalishaji na usambazaji wa mbegu.

Kwa sasa, dunia inakabiliana na msukosuko mkubwa wa afya utokanao na mlipuko wa virusi vya corona. Mashirika ya Afya na serikali zote ulimwenguni zimechukua tahadhari mbalimbali kudhibiti kuenea kwa virusi hivi. Rijk Zwaan inatambua athari za jambo hili na inachukua hatua madhubuti.

Tunajali usalama wa wafanyakazi na washirika wetu wa kibiashara

Kwa kifupi tu ni kwamba, usalama wa wafanyakazi wetu, washirika na wanunuzi wa mbegu zetu ni tunalipa kipaumbele cha juu kabisa. Tunafuatilia kwa umakini mkubwa ushauri unaotulia na mashirika ya afya na serikali husika katika kila nchi, na kutekeleza hatua hizo ndani ya kampuni kwa jinsi inavyopaswa.

Mboga na mbegu za mboga ni msingi wa uhakika wa chakula

Mbegu za mboga kwa sehemu ni mhimili wa mnyororo wa chakula unaotengeneza msingi wa ulaji wa aina tofauti wenye kuleta afya njema. Bila mbegu za mboga, wakulima hawawezi kuzalisha hivyo watu watu watakosa mboga za kula. Tukiwa kama kampuni ya uahamili wa mboga, kwa sasa tunafahamu jukumu letu na umuhimu wa suala hili kupita wakati mwingine wowote ule – kwa pande zote mbili tukiwa kama sekta na kampuni pia – katika tasnia ya ugavi wa chakula dudiani.

 Mapema wiki hii, Shirikisho la Mbegu la Kimataifa lilichapisha tangazo thabiti linalosisitiza umuhimu wa kutokuweka vikwazo kwenye usafirishaji wa mbegu kimatifa ili kuhakikisha uwepo wa uhakika wa chakula, na kuziomba serikali kuwezesha jambo hili kwa ufanisi wa hali ya juu.

Tunazingatia mahitaji ya wateja

Kila siku wafanyakazi wetu wanafanya kila linalowezekana kutimiza mahitaji ya wateja wetu na kuhakikisha mbegu za mboga zinawafikia kama ilivyopangwa. Tunaendelea kufikiria kwa pamoja jinsi ya kupata suluhisho la changamoto zinazowakabili washirika na wateja wetu katika kipindi hiki cha janga la virusi vya corona. Unaweza kututegemea, endelea kutuamini.

Tafadhali tuendelee kusaidiana. Kwa pamoja, tutashinda!

Marco van Leeuwen, Ben Tax and Kees Reinink

Bodi ya Wakurugenzi, Rijk Zwaan