SSA | Hero | VI24 | Jacqueline

Simulizi - 26-10-2017

Huu ndiyo muda muafaka wa kuwekeza

Jacqueline Mkindi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kilimo cha Bustani cha Tanzania, ambacho huwakilisha wakulima 25,000 kote nchini. Lengo lake ni kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo cha bustani. Kwa vile sasa kuna msukumo mkubwa, yeye anahimiza kwamba huu si wakati wa kulegea. Jacqueline Mkindi ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cah Kilimo cha Bustani Tanzania (Tanzania Hoerticultural Association – TAHA) kinachowakilisha wakulima 25,000 nchini kote. Lengo lake ni kukuza na kuendeleza tasnia ya kilimo cha bustani. Kwa vile sasa gurudumu linakaza mwendo, anashauri kwamba huu si muda wa kulegeza kamba.

Mwamko zaidi

 “Tanzania ina uwezo mkubwa, hususan katika kilimo cha bustani. Kwa hali ya hewa tuliyo nayo tunaweza kulima kitu chochote, na tunashuhudia ongezeko la utashi wa kisiasa pia. Watu wanakuwa na mwamko zaidi kuhusu ubora, ubichi (freshness) na usalama wa chakula. Majani ya saladi (lettuce)  yanaleta matumaini kutokana na  soko zuri la sekta ya utalii na hoteli.”

Miundombinu

“Ingawa malengo mengi yametimiza, bado kuna kazi nyingi za kufanya. Nazungumzia haja ya kuinua tija, upatikanaji wa mikopo na upangaji na uboreshaji wa miundombinu. Vyote hivi vinahitajika ili kuwafikia wakulima wadogo. Tusipowekeza sasa tunaweza kupunguza kasi yetu.”

Ushirikiano

“Tumehamasika kuboresha mtandao wetu wa ugavi kupitia vitengo vyetu vya biashara vya TAHA Fresh na Fresh 2 Sokoni. Katika miradi hii miwili, pamoja na TAHA yenyewe, tunaona umuhimu wa ushirikiano. Ili kuwafikia wakulima wadogo wengi iwezekanavyo tunahitaji msaada wa makumpuni makubwa – iwe wauzaji wan je, wasindikaji, wajenzi wa greenhouses ou wagavi wa vifaa vya bustani – kwa vile wana utaalam nauwezo ambao tunauhitaji.”


Hivi majuzi nilitembelea Rijk Zwaan huko Uholanzi. Niliona uwekezaji mkubwa, majengo na vifaa, na wafanyakazi mahiri – nilishawishika sana! Bila shaka tunahitaji mbegu bora zaidi ili kuibadili tasnia yetu, lakini kuna mabadiliko mengine ambayo pia tunapaswa kuyafanya. Rijk Zwaan pia walinionyesha ule mnada wa ubelgiji, kama mfano mmojawapo ya ushirikiano, na viwango vya ubora wanavyotumia. Kujifunza kutoka kwa wengine ni kitu chema sana. Kama nchi tunapaswa kufunguka, tunahitaji kila msaada tunaoweza kupata.”