SSA | Media | Hero | VI24 | Personal advice

Ushauri binafsi

Mbegu zetu chotara zinalenga mahitaji maalumu ya mahali husika kwa kuzingatia hali ya hewa na mahitaji ya soko. Ustahimilivu dhidi ya wadudu na magonjwa unamaanisha kwamba mahitaji ya matumizi ya viuatilifu huwa madogo zaidi na hivyo kuongeza tija katika kilimo.

Hata hivyo, ili kufanikiwa katika kilimo cha mboga chotara, wakulima wanahitaji mafunzo ya kina ya kitaalam. Kwa sababu hiyo, pamoja na mambo mengine wataalam wetu wa mazao na washauri wa masoko hutoa ushauri maalum kuhusu siku za kupanda, utunzaji wa mimea, mahitaji muhimu na uwekezaji wa ziada. Kwa njia hii tunawasaidia wakulima kupata mavuno mengi iwezekanavyo kulingana na aina husika.

Unaweza kutarajia nini kutoka kwetu?

 

  • Wigo mpana wa aina za mbegu kwa mahitaji mbalimbali
  • Kutembelewa na wataalamu wa Rijk Zwaan au washirika wa Rijk Zwaan
  • Mialiko ya kutembelea mashamba yetu ya maonyesho ili uweze kupata mawazo na mbinu mpya na mbadala
  • Miongozo ya kilimo na taarifa za majaribio
  • Maelekezo ya jinsi ya kukadiria faida kutokana na uwekezaji wako

undefined

Ongezeko la kuvutiwa na ubora wa mboga

Dokun Ogunbodede anamiliki kampuni ya biashara ya kilimo nchini Nigeria, ambapo yeye huchanganya uzalishaji mboga, ushauri na maoni ya usambazaji ya wakulima wengine. Kwa kipindi cha miaka michache iliyopita, amekuwa akifanya kazi na Rijk Zwaan. Pamoja, wanaona uwezo mkubwa wa kilimo nchini Nigeria.