SSA | Hero | VI24 | The story of Elijah (SEVIA)

Simulizi - 26-10-2017

Pamoja tunajaribu kuziba pengo la maarifa

Elijah Mwashayenyi ni mkurugenzi mtendaji wa SEVIA, taasisi ya ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi inayolenga kuendeleza biashara ya mboga barani Afrika kwa kuingiza teknolojia na aina za mboga chotara na pia kuwaongezea wakulima maarifa ya kiufundi.

Kukua taratibu

“Tumeweka malengo ya juu: tunataka tuwe tumewafikia wakulima 30,000 nchini Tanzania ndani ya miaka mitano. Ili kuweza kuwafikia watu wengi kiasi hicho tunatumia maafisa ugani, kila mmoja wao akiwa na eneo maalum. Kila afisa ugani ana takriban mashamba darasa 15 , ambayo anafundishia makundi na watu binafsi. Tunachagua ‘wakulima viongozi’ ambao wanatekeleza jukumu muhimu kwenye jamii zao na kuwapa mfunzo ya ziada, na baada ya msimu mmoja wa mafunzo tunahamia kijiji kingine ili tuweze kuwafikia wakulima wengi iwezekananvyo.”

Kuchangia utaalam

 “Katika nchi kubwa kama hii lazima tuweke vipaumbele. Tunafanya hivyo pamoja na washirika wetu: Rijk Zwaan, East West Seeds na idara ya utafiti wa mimea ya kituo cha utafiti cha chuo kikuu cha Wageningen. Michango ya fedha na utaalam kutoka Rijk Zwaan inasaidia wakulima wote na si wale wanaonunua mbegu za Rijk Zwaan tu, kitu ambacho si kawaida. Tunakaa chini, tunaangalia pengo lililopo la ujuzi na tunajaribu kutumia utaalam tulio nao kulijaza. Kwa mfano, tunaweza tukahitaji kuanzisha mradi mpya wa utafiti au kuanzisha aina mpya ya mafunzo.

Mageuzi

“Changamoto moja kubwa kwa kilimo cha bustani barani Afrika ni kubadilisha mtazamo. Tofauti na kilimo cha nafaka, wakulima wa mboga wanapaswa kuwa na mtazamo wa soko kwanza, wajipange na waone mboga kama biashara. Kwa ajili hiyo huwa tunawaelekeza kwenye Chama cha Kilimo cha Bustani Tanzania (Tanzania Horticultural Association – TAHA), ambako wanaweza kupata msaada wa masoko, ikiwa pamoja na fursa za kuuza mazao yao nchi za nje. Lakini pia kuna upande mwingine. TAHA inaweza kuwaelekeza wakulima Rijk Zwaan kupata ushauri kuhusu greenhouses. Na Rijk Zwaan kwa upande wake ikawaelekeza wakulima SEVIA kwa ushauri wa kitaalam. Ni kama mduara wenye lengo moja: kufundisha idadi kubwa ya wakulima ikiwa kitu kimojawapo, lakini kuasili (kwa teknolojia) na ‘mageuzi ya kijani’ vikiwa ndoto yenyewe.”